Kipa namba moja wa Gor
Mahia, Boniface Oluoch aliyekuwa anawaniwa na Simba, ameibuka na kuwa kipa bora
wa michuano ya Kagame.
Oluoch ameshinda tuzo
hiyo iliyokuwa ikipewa kura nyingi kwenda kwa kipa wa Azam FC, Aishi Manula kwa kuwa timu yake imebeba ubingwa bila kufungwa hata bao moja.
Manula hajafungwa hata
bao moja katika mechi zaidi ya nne alizocheza, huku Gor Mahia ikiwa imeruhusu
mabao 6.
Oluoch amesema
anafurahia tuzo hiyo inayozidi kumpa changamoto zaidi ya kufanya vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment