Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesogeza mbele kufungwa kwa
dirisha la usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) mpaka Agosti 20 mwaka huu.
Awali, dirisha la usajili lilikua lifungwe leo Agosti 6, na usajili mdogo
wa ndani ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa jumla
utafungwa Agosti 20, 2015.
Tarehe 21- 28 Agosti, 2015 ni kipindi cha pingamizi, tarehe 29-30 Agosti
2015, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.
Dirisha la uhamisho wa wachezaji wa Kiamataifa (FIFA –TMS) litafungwa
tarehe 06 Septemba, 2015 na Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua
vumbi Septemba 12, 2015.
TFF inavitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda huo uliowekwa,
ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha
litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi
Novemba 15 mwaka huu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment