August 15, 2015


Najua uliwahi kuisikia ile stori ya Steve Yanga kumwaga chozi baada ya Yanga kutundikwa mabao 5-0 na Simba, kuanzia bapo akawa maarufu.


Sasa Steve amehamia Azam FC ambao ndiyo mabingwa wa Kombe la Kagame.
DIAMOND AKIWA NA WAZAZI NA WADODGO ZAKE WAKIWASILI UTURUKI 
Lakini stori nyingine tamu ya kuvutia ni ya kijana Louis Diamond mwenye umri wa miaka mitano ambaye alimwaga chozi baada ya kuona mshambuliaji Robin van Persie akihama Manchester United na kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki.

Picha za video za Diamond akilia zilisambaa kwa kasi kubwa mtandaoni na wengi walionekana kumuonea huruma.
SIKU ALIPOMWAGA CHOZI

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Fenerbahce uliamua kumpa nafasi Diamond ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Manchester United pamoja na familia yake kutembelea Uturuki ili apate nafasi ya kumuona van Persie ambaye ni shujaa wake.

Diamond amepewa ofa ya kukaa Istambul kwa siku tano akiwa katika hoteli bomba kabisa, akiwa na wazazi wake watamuona van Persie ikiwa ni pamoja na kupata nafasi nyingine ya kuona mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Uturuki, van Persie akiwa uwanjani anaichezea Fenerbahce.

VAN PERSIE AKIWA KAZINI UTURUKI
FERNABAHCE.COM




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic