August 20, 2015

Simba iko katika hatua za mwisho kumalizana na mshambuliaji hatari kutoka Senegal ambaye anatarajia kutua nchini ndani ya siku mbili zijazo.


Papa Niang, raia wa Senegal aliyezaliwa Desemba 5, 1988, sasa ana miaka 26 atatua nchini kumalizana na Simba.

Mara ya mwisho alikuwa akiichezea CF Monana ya Gabon ambayo alijiunga nayo akitokea Al Shaabab ya Kuwaita, moja ya timu tajiri katika Ukanda wa Ghuba ya Uajemi.

Habari za ndani ya Simba zinaeleza Niang anakuja nchi kumalizana na uongozi wa Msimbazi baada ya kuwa imekubaliana naye kila kitu.

"Ni kweli, kuna mtu alipewa kufanya kazi hiyo ya Niang na mambo yamekwenda vizuri, sasa anakuja nchini na anamalizana na uongozi.

"Viongozi wamekuwa wakilishughulikia hilo kwa kasi kubwa ili kuwahi dirisha la usajili," kilieleza chanzo cha uhakika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic