Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza kikosi cha
timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U13) kitakacho kuwa
jijini Mwanza kujiandaa na fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 17 mwaka 2019 nchini Tanzania.
Mapema mwezi Juni mwaka huu TFF iliandaa mashidano ya Taifa ya
vijana yaliyofanyika jijini Mwanza ambapo japo la makocha chini ya Idara ya
ufundi ya TFF, waliweza kuchagua vijana wenye vipaji ambao wanaunda timu hiyo.
Vijana
hao wenye vipaji watakua wakiishi, kufundishwa mpira na kusoma katika shule ya
Alliance iliyopo jijini Mwanza ambayo TFF imeingia mkataba na shule hiyo kwa
ajili ya kuwalea wachezaji hao na kuendeleza vipaji vyao.
Mpango
huo wa kuandaa kikosi cha vijana utafanyika pia mwakani kwa kuchagua vijana
wenye umri chini ya miaka 14 (U14), na mwaka unaofuata kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 15 (U15) kwa lengo la kuendelea kuboresha kikosi hicho cha
vijana.
Wachezaji
waliochaguliwa kujiunga na timu hiyo ya vijana ni Jaffar Juma (Arusha),
Moris Michael (Ilala - Dsm), Jonathan Raphael (Kasulu – Kigoma), Karim Mfaume
(Lindi), Erick Buyaga (Nyamagana – Mwanza), Shabani Kimwaga (Kinondoni – Dsm),
Feisally Awadh (Ilala – Dsm), Abdulatif Noor (Tanga), Edmond Godfrey (Geita) na
Adam Selemani (Kibaha – Pwani).
Wengine
ni Selaman Juma (Kibaha – Pwani), Wilbert John (Ilala – Dsm), Ahsante Hamisi
(Kinondoni – Dsm), Isaya Ernest (Mbeya), Gasper Gombanila (Nyamagana – Mwanza),
Joseph Awadh (Ilala – Dsm), Alfonsi Mabula (Nyamagana - Dsm), Cosmas
Lucas (Nyamagana – Mwanza), Haroub Juma (Bariadi – Simiyu) na Ladak Juma
(Morogoro).
Wakati
huo huo wachezaji watano kutoka kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri
chini ya miaka 15 (U15) wanatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu wa
Agosti kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio katika klabu ya
vijana ya Orlando Pirates.
Nafasi
hiyo imepatikana kufuatia mazungumzo ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Rais wa
klabu hiyo Irvin Khoza kuomba vijana hao kupata nafasi ya kufanya majaribio
katika klabu hiyo na endapo watafuzu, watajiunga na timu ya vijana ya Orlando
Pirates.
Wachezaji
hao ni Asaad Ali Juma (Zanzibar), Maziku Amaan (Dodoma), Issa Abdi (Dodoma),
Kelvin Deogratias (Geita) na Athumani Maulid (Kigoma) wataongozana na
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi kuelekea Afrika Kusini Agosti 28,
2015 kwa ajiliya kufanya majaribio hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment