August 17, 2015


Timu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga, jana Jumapili ilifanikiwa kuifunga Friends Rangers ya jijini Dar kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Karume, Dar.


Friends ambayo ilikuwa ikiongozwa na kiungo wa zamani wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ pamoja na straika aliyeachwa na Yanga, Jerry Tegete, walishindwa kuibeba timu hiyo na kukubali kipigo hicho kutoka kwa vijana wa Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ waliokuwa na wachezaji wao mahiri, Jabir Aziz ‘Stima’, Nizar Khalfan na wengineo waliojiunga na timu hiyo hivi karibuni.

Mabao ya Mwadui yalifungwa na Fabian Gwise dakika ya 59 na Stima (75) huku lile la kufutia machozi la Friends likiwekwa kimiani na Tegete (88). Kocha wa Mwadui, Julio muda wote alikuwa akimtania, Herry Mzozo ambaye anainoa Friends kwa kumuambia mechi hiyo ameroga kutokana na wachezaji wake kukosa mabao ya wazi ambayo anaamini wangewafunga mengi tu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic