Yanga itashuka dimbani
Jumapili kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya City.
Mechi hiyo itapigwa
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Kuu
Bara.
Yanga imeweka kambi
mjini Tukuyu kujiandaa na ligi kuu, na tayari imeshacheza mechi moja ya
kirafiki dhidi ya Kimondo ya Mbozi na kushinda kwa mabao 4-1.
Kabla ya mechi hiyo ya
Jumapili, Yanga inatarajia kushuka dimbani kesho kucheza na Prisons ya Mbeya.
0 COMMENTS:
Post a Comment