August 19, 2015

MAGURI AKIPAMBANA...

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Elias Maguri aachwe ndani ya kikosi hicho, kocha wake, Muingereza, Dylan Kerr, ametoboa siri iliyokuwa nyuma ya pazia la sakata hilo kwa kusema kuwa, mshambuliaji huyo alimfuata akitaka kuondoka.

Maguri ambaye alitua Simba na kupewa mkataba wa miaka miwili akitokea timu ya Ruvu Shooting, ameachwa ndani ya kikosi hicho baada ya uongozi wa klabu hiyo kumsitishia mkataba wake ambapo kwa sasa ni mchezaji huru licha ya kuripotiwa kwamba ana mipango ya kurejea kwenye timu yake ya zamani.

Kerr ambaye ni beki wa zamani wa kushoto wa timu ya Kilmarnock ya Scotland, amesema alikubali kumruhusu mshambuliaji huyo kuondoka ndani ya kikosi hicho kutokana na yeye kumfuata na kuomba ruhusa ya kuondoka kutokana na kuona mambo yanakuwa mabaya kwake.
KERR

“Maguri mwenyewe alinifuata na kuniambia juu ya suala lake hilo la kutaka kuondoka, sikuwa na tatizo na sikuwa na sababu ya kumpinga kutokana na nafasi yake kikosini kuwa ndogo, ukilinganisha na washambuliaji wengine waliopo,” alisema Kerr ambaye ni shabiki mkubwa wa Manchester United ya Uingereza.


Hivi karibuni, Maguri alikuwa akilalama kwamab hajui mustakabari wake ndani ya kikosi cha Kerr baada ya kuondolewa siku moja kabla ya Simba Day.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic