August 16, 2015


Kiungo Javier Mascherano wa Barcelona amesema licha ya kupigwa mabao 4-0 na Athletico Bilbao, ana imani kubwa bado wana nafasi ya kubeba Super Cup ya Hispania.


Barcelona ilitwangwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ikiwa ugenini. Sasa inasubiri mechi ya marudiano.

Akizungumza na waandishi wa habari, MAscherano ambayo ni mmoja wa manahodha wa Barcelona, amesema watapambana hadi mwisho.

"Hatuwezi kwenda uwanjani tukiamini tumepoteza, tunaamini bado tuna nafasi na tutapambana.

"Kweli kuna ugumu, lakini lazima tucheze kwa uwezo wa juu na juhudi za juu zaidi," alisema raia huyo wa Argentina.

Barcelona itakuwa mwenye wa Bilbao katika mechi ya marudiano na inatakiwa kushinda mabao 5-0 ili kubeba kombe hilo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic