August 17, 2015

MAGURI
Uongozi wa Simba, leo umetangaza rasmi kuachana ana mshambuliaji wake Elius Maguri pamoja na kipa Ivo Mapunda.


Tayari SALEHJEMBE iliandika kuhusiana na kutemwa na Maguri, lakini uongozi wa Simba umeweka hadharani.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema Kocha Mkuu, Dylan Kerr ndiye alitoa mapendekezo.

“Tunaheshimu mapendekezo ya kocha Kerr na sasa Maguri ni mchezaji huru na tumemalizana vizuri sana,” alisema Manara.
Dalili za Maguri kuachwa Simba zilianza baada ya kuondolewa kwenye Simba Day.

Hali hiyo ilionyesha kumshangaza, lakini uongozi wa Simba uliendelea kuwa kimya hadi ulivyotangaza leo.
 
IVO
Kuhusiana na Ivo, yeye tayari alishapewa fedha za usajili. Lakini uongozi wa Simba umemueleza kwamba hakuwa na ushirikiano wakati akitafutwa kusaini mkataba.

Wakati fulani Ivo aliwahi kushutumu kuhusiana na vyombo vya habari kuwa vinadai haonekani na anatafutwa kusaini mkataba jambo ambalo halikuwa kweli na uzushi mtupu.


Lakini ndiyo jambo aliloelezwa na uongozi wa Simba leo, kwamba hakuwa na ushirikiano, hivyo anaweza akaendelea na mambo yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic