Kikao cha Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF ) kilichokutana mwishoni mwa wiki jijini
Cairo nchini Misri, kimewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake
mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.
Walioteuliwa pamoja na kamati zao
katika mabano ni:
1. Leodeger Tenga- (Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya
Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani
(CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya
Ushauri na Vyama Wanachama).
2. Jamal Malinzi - (Mjumbe kamati
ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)
3. Mwesigwa Selestine - (Mjumbe
Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).
4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe
Kamati ya Rufaa)
5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati
ya Tiba)
6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la
Wanawake)
7. Crescentius Magori-(Mjumbe
Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)
Shirikisho la Soka Tanzania - TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati
mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
TFF.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA
WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment