Rais wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za rambi rambi kwa Rais wa
Chama cha Soka nchini Malawi (FAM), Walter Nyamilandu kufutia kifo cha aliyekua
Rais wa chama hicho John Zingale.
John Zangale alifariki dunia baada
ya kuugua kwa muda mfupi wiki iliyopita katika hospitali ya Mlambe
iliyopo Blantyre nchini Malawi na kuzikwa mwishoni mwa wiki alikuwa Rais wa FAM
mwaka 1998- 2002.
Katika salam zake kwenda kwa Rais
wa FAM, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu pamoja na chama cha soka
nchini Malawi kwa msiba huo, na kusema TFF kwa niaba ya Watanzania iko pamoja
nao katika kipindi hicho cha maombelzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment