Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga
Stars) iliyopo kambini kisiwani Zanzibar, inatarajiwa kucheza mchezo wa
kirafiki na timu ya taifa ya Wanawake kutoka Kenya (Harambee Starlets) Agosti
23, 2015.
Mchezo huo wa kirafiki utachezwa katika uwanja wa Aman
Kisiwani Zanzibar, ikiwa ni sehmu ya maandalizi ya kikosi hicho kujiandaa na
fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika nchini
Congo-Brazzavile kuanzia Septemba 4 – 19, 2015.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi kutwa mara mbili
katika viwanja vya Aman na Fuoni chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage
kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, wachezaji wote waliopo kambini
wapo katika hali nzuri wakiendelea kujifua na michezo ya Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment