Dirisha
la usajili limeongezwa toka tarehe 06 Agosti hadi tarehe 20 Agosti, baada ya
muda huo klabu itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha
shilingi laki tano (Tsh 500,000) kwa kila mchezaji itakayemsajili mpaka siku ya
tarehe 30 Agosti.
Mwisho wa
kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni tarehe 6
Septemba.
Kikao cha
kamati ya sheria kitakaa tarehe 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa
tena tarehe 8/9/2015 kwa ajili ya kupitisha usajili.
Kuanzia
tarehe 21 hadi 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF
Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi
kuwawekea wachezaji mapingamizi.
Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza tarehe 12 Septemba 2015, Daraja la kwanza
(FDL) ikitarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba
16 mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment