August 21, 2015




Klabu  ya Mbeya City imemwaga kitita cha Sh milioni 6 kwa mkataba wa miezi sita iliosaini na kipa Juma Kaseja.


Kaseja ametua Mbeya City akiwa mchezaji huru baada ya kuhitilafiana na Yanga ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.

Katika mkataba huo, Mbeya City wamemlipa Kaseja Sh milioni 6 kama ada ya usajili na tayari mkataba umesainiwa juzi usiku jijini Dar es Salaam ambapo mshahara wake utakuwa ni Sh milioni moja kwa mwezi, hivyo kama ukigawa fedha zake za usajili, ukajumlisha na mshahara, thamani yake itakuwa ni Sh milioni mbili kila mwezi.

“Mshahara utakuwa ni shilingi milioni moja, unajua Juma ni mchezaji mkongwe, hivyo tumeamua kumpa heshima yake ili ashirikiane na wenzake vizuri,” kilieleza chanzo kutoka Mbeya City.

“Lengo ni kujiimarisha zaidi, hivyo uongozi umefikia uamuzi huo na tunaamini atakuwa na mchango mkubwa kutokana na ukongwe wake.”

Mbeya City imekuwa ni timu ya nne kwa Kaseja kuichezea katika Ligi Kuu Tanzania Bara, kwani alianza na Moro United, Simba, Yanga kabla ya kutua City.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic