Arsenal imeshinda bao 1-0
dhidi ya Chelsea na kubeba Ngao ya Hisani hata ukipenda ya Jamii, hehe.
Bao hilo la Oxlade-Chamberlain
limeipa Arsenal heshima na kuvunja ule mwiko wa kushindwa kuifunga Chelsea
ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Safari hii Kocha Arsene
Wenger ameibuka kidedea kwa kuitwanga Chelsea, lakini akalipa kisasi kingine.
Najua utauliza kipi? Amegoma
kumpa mkono Mourinho, dakika kabla mechi haijaisha, huyooo akaingia zake
vyumbani kama Mourinho ambavyo amekuwa akimfanyia.
0 COMMENTS:
Post a Comment