August 18, 2015


Baada ya kutembeza vipigo mkoani Mbeya, Yanga  imerejea jijini Dar es Salaam na kuanza kambi.


Kambi hiyo ni maandalizi ya mwisho kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Yanga ilikuwa Mbeya ambako ilianza mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Kimondo ya Mbozi na kuitwanga kwa mabao 4-1.

Baada ya hapo ilikutana na Prisons na kuchaopa mabao 2-0 kabla ya kuituliza Mbeya City kwa mabao 3-2.


Sasa Yanga imerejea kumalizia kambi yake jijini Dar es Salaam kabla ya kuivaa Azam FC wikiendi hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic