August 18, 2015


CANNAVARO
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', Oscar Joshua na mshambuliaji Amissi Tambwe ni wagonjwa.


Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro amesema watatu hao wanasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

"Kweli malaria inawasumbua na matibabu yanaendelea, lakini kocha amewataka waingie kambini.
"Tutakuwa nao, mambo yatakwenda vizuri tunaamini. Watapata nafuu na ikiwezekana kuungana na wenzao kuisaidia Yanga," alisema Muro.

Kuhusiana na maandalizi mengine kabla ya kuivaa Azam Fc wikiendi, Muro alisema kila kitu safi.

"Maandalizi yanakwenda vizuri kabisa na kambi ya Dar es Salaam ni ya mwisho kabla ya kuivaa Azam FC," alisema.

.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic