September 4, 2015

JEZI AMBAZO IMEKUWA IKITUMIA...

Timu za Ligi Kuu Bara zilikabidhiwa jezi na vifaa kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo, Kampuni ya Vodacom, juzi, lakini imebainika kuwa Azam FC haitavitumia.


Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema timu yake imekuwa ikifanya hivyo kwa misimu kadhaa.

Ingawa hakutoa sababu za kina juu ya maamuzi yao hayo lakini alifunguka hivi:

“Huwa hatuzitumii hizo jezi, msimu wa pili sasa tunatumia jezi zetu wenyewe, cha msingi ni kufuata utaratibu unavyotakiwa, kama vile kuwepo kwa nembo ya mdhamini kwenye sehemu husika ya jezi na mambo mengine, ndiyo maana tunatumia za kwetu wenyewe na hakuna tatizo.


“Zile jezi tunazopewa na mdhamini mara kadhaa huwa tunazigawa kwa timu zetu za vijana au kwingine, hata zile za mazoezi kama bips tunazopewa pia hatuzitumii, tunatumia tunazotengeneza wenyewe na ni kwa sababu tunapenda zaidi kutumia vya kwetu wenyewe.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic