September 4, 2015


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Malimi Busungu, amejikuta akishinda chumbani kwake muda mwingi akitafakari maelezo ya kocha wake, Hans van Der Pluijm ambaye amemtaka kujifunza kupambana na kutokata tamaa.


Busungu amefikia hatua hiyo baada ya kuonekana kukata tamaa kutokana na ushindani mkali wa namba uliopo kikosini hapo.

Pluijm aliamua kumpa darasa kubwa mchezaji huyo ambaye ametua Yanga hivi karibuni akitokea Mgambo ya Tanga, baada ya kuona makali yake yanapotea.
 Busungu alisema: “Aliniambia mambo mengi sana na mengine kwa faida yangu lakini kikubwa alikuwa akinitaka niongeze bidii mazoezini kwani ana imani na mimi, pia nisisikilize maneno ya watu wa nje ambayo wamekuwa wakisema juu yangu.

“Hakika hali hiyo ilinifanya nitumie muda mwingi baada ya mazoezi nikiwa chumbani kwangu nikitafakari moja baada ya jingine, kusema kweli Pluijm ni bonge la kocha na sasa najiona kama nimezaliwa upya, hivyo ngoja ligi ianze.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic