Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi
leo amefunga fainali za michuano ya kombe la Airtel Rising Stars katika uwanja
Karume jijini Dar es Salaam.
Akiongea kwakati wa ufungaji michuano ya airtel mbele ya halaiki
ya vijana walioshirki michuano hiyo, Malinzi ameishukuru kampuni ya simu ya
Airtel kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo inawapa nafasi vijana ya
kucheza mpira na kuonekana na baadae kujipatia ajira.
“Lengo
la TFF ni kushirki fainali za Olimpiki za Dunia mwaka 2020 Tokyo –Japan hivyo
wachezaji wenye vipaji kutoka kwenye michuano hii ya Airtel na vijana wengine
wataendelea kutunzwa kwa ajili ya timu ya Taifa ya baadae” Alisema Malinzi.
Naye
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao ndio wadhamini
wakuu wa michuano hiyo, amesema airtel wataendelea na program hiyo ya vijana
wenye umri chini ya miaka 17 kwa wanawake na wanaume, na kuahidi kuendelea
koboresha michuano hiyo kila mwaka.
Michuano
ya Airtel Rising Stars iliyomalizika leo, ilizisihirkisha timu za wanaume na
wanawake kutoka mikoa saba nchini, huku mashindano hayo yakiwa yanafanyika kwa
msimu wa tano sasa tangu kuanzishwa mwaka 2011.
Kwa
upande wa wanaume, timu ya Ilala imeibuka mabingwa baada ya kuifunga Mbeya kwa
mabao 4-0 katika mchezo wa fainali ulochezewa jioni ya leo, huku timu ya
wanawake ya Temeke wakiibuka washindi baaada ya kuibwaga Kinondoni mwa mikwaju
ya penati 5-4.








0 COMMENTS:
Post a Comment