September 11, 2015


Usajili wa Simba uko vizuri na uliopangiliwa kama unavyotakiwa, tofauti na watu wengi wanavyofikiria.


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema ana imani na kikosi chao.

"Usajili wa Simba umekwenda kisayansi, tumesajili karibu kila mtu kwa kufuata utaratibu, mfano tumesajili wachezaji wawili wawili kwa kila nafasi.

"Pia tumeangalia mwalimu anataka nini na sisi tukatekeleza. Hivyo naamini ni usajili sahihi kabisa kiufundi na hakuna hofu kwa kuwa kila kitu kilifuata utaratbu na matakwa sahihi ya benchi la ufundi," alisema.

Hans Poppe amesema Simba ilifanya usajili wa kisayansi ukilinganishwa na timu nyingine.

Katika usajili wake, Simba imefanikiwa kuwarejesha wachezaji wake wawili wakongwe, Mwinyi Kazimoto aliyekuwa Al Markhiya ya Qatar pamoja na Mussa Hassan Mgosi aliyekuwa akiitumikia Mtibwa Sugar.

Simba inaanza ligi kesho kwa kuwavaa African Sports ikiwa ugenini mjini Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic