September 12, 2015


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi,amewakomalia wagombea urais Tanzania kuhakikisha wanaikumbuka michezo hasa soka pindi mmoja wao atakaposhinda nafasi hiyo.

Kauli hiyo ya Malinzi imeenda moja kwa moja kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli na Edward Lowassa kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Magufuli na Lowassa ndiyo wenye nguvu ya kisiasa kwa sasa na kuna uwezekano mkubwa mmoja wao akashinda kiti cha urais.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema yeyote atakayeshinda nafasi ya rais anatakiwa kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya soka ili kuifanya Tanzania itambe kimataifa.

“Niwaombe tu wagombea wa urais, Magufuli na Lowassa kama mmoja wao akifanikiwa kuingia madarakani basi asitusahau wanamichezo kwani tunahitaji viwanja vya soka kwani vilivyopo ni vichache,” alisema Malinzi.


“Hata kama wakishindwa kujenga vipya bali vile vilivyopo wavisimamie kwenye ukarabati kwani kama hilo likifanikiwa naamini michezo itapiga hatua nchini.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic