![]() |
| MAREHEMU AKIWA NA MJUKUU WAKE, ANDY AMBAYE NI MTOTO WA KWANZA WA MOLANDI. |
Mwandishi mwandamizi
wa gazeti la Championi, Wilbert Molandi amepata msiba mkubwa wa kufiwa na baba
yake mzazi.
Andrew Molandi amefariki
dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mzee Molandi
amefariki dunia baada ya kuugua kwa siku kadhaa na mipango ya mazishi inafanywa
nyumbani kwake Kigogo jijini Dar es Salaam.
Molandi
ameiambia SALEHJEMBE, wako katika hatua za mwisho kuhusiana na maziko ya mzee
wake.
“Ndugu
tunakutana kwa ajili ya kujadili na baada ya hapo tutatoa taarifa kama mwili
utasafirishwa au tutazika hapa Dar es Salaam,” alisema Molandi.








0 COMMENTS:
Post a Comment