Bondia Floyd Mayweather amesisitiza kwamba Andre Berto ndiye
bondia wa mwisho kupigana naye katika pambano lao la Jumamosi.
Amesema tofauti na wengi wanavyamini atapigana tena, pambano
hilo la 49 ndiyo litakuwa la mwisho kwake na anataka kushinda kubaki na rekodi
yake ya kutopigwa daima katika ngumi za kulipwa.
Pambano hilo litafanyika katika Ukumbi wa MGM Grand Garden jijini
Las Vegas, Marekani na tayari tiketi zimeanza kuuzwa na zinakaribia kwisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment