Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans
Poppe amesema amemaliza kazi yake na ameishakabidhi mikoba kwa kamati nyingine.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Hans Poppe amesema kuwa baada ya
kukamilisha usajili, amekabidhi kila kitu kwa kamati ya ufundi na ile ya
mashindano.
“Kazi ya kamati ya usajili imeisha, tumeishakabidhi kila
kitu kwa kamati ya ufundi na ile ya mashindano.
“Tunachosubiri sasa ni kuanza kwa ligi, hapo tunaweza tukawa
tunaangalia mambo mbalimbali ya kufanya na nini tusaidie,” alisema Hans Poppe.
Simba ni kati ya timu zilizofanya usajili mkubwa kwa ajili
ya msimu ujao na sasa inachosubiri ni kuanza tu kwa ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment