September 11, 2015


Siku chache baada ya kuonekana katika mazoezi ya Azam FC, kipa mkongwe Ivo Mapunda, juzi Jumatano alionekana katika mazoezi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba akiwanoa makipa wa timu hiyo.


Kipa huyo wa zamani wa Yanga na Simba, alionekana akiwa bize muda mwingi ambapo alisema kuwa yupo Mwanza kwa mapumziko ya wiki moja.

“Nimekuja kupumzika lakini kwa kuwa mimi ni mchezaji, nimeona siyo mbaya nikifanya mazoezi na wenzangu, natagemea kuondoka Ijumaa (leo) kurejea Dar es Salaam ambako nitafanya mazoezi na Azam FC,” alisema Ivo.


Awali, Ivo alialikwa kwenda kufanya mazoezi katika kikosi cha AFC Leopards cha Kenya kinachonolewa na kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Loagarusic.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic