Baada ya beki wa kulia wa Taifa Stars, Shomari Kapombe kuonyesha
soka maridadi juzi Jumamosi na kufanikiwa kuwadhibiti washambuliaji wa Nigeria,
hasa staa wa KAA Gent ya Ubelgiji, Moses Simon, amefunguka kuwa kilichomsaidia
ni akili nyingi tu, wala si kingine.
Katika mchezo wa juzi Jumamosi kufuzu Afcon 2017, Kapombe
alionekana kuwa makini muda wote na kufanikiwa kudhibiti mashambulizi ya hatari
yaliyotaka kuundwa kutokea upande wake kupitia kwa winga Moses kabla ya winga
huyo kuonekana kufeli na kocha wake, Sunday Oliseh kuamua kumtoa kwenye dakika
ya 69 na kumuingiza Edouk Samuel.
KAPOMBE AKIWA NA GWIJI WA ZAMANI ARSENAL, WILLIAM GALLAS |
“Unajua kilichotokea pale ni kugundua unahitaji kutumia nini kwa
mshambuliaji kama yule, yeye anatoka kwenye ligi za kimataifa na ashakutana na
changamoto ya mabeki wengi wazuri, kwa hiyo ana changamoto ya kutosha,
kilichohitajika ni umakini mkubwa juu yake na kucheza kwa akili kubwa.
“Hiyo ndiyo ilikuwa silaha yangu, nilimchezea kwa akili sana
lakini pia ujanja na mbinu tulizopewa na kocha Mkwasa (Boniface) zilisaidia
kujiamini na kucheza vile, ndiyo maana unaona safu yetu ya ulinzi kwa ujumla
ilitulia, nafikiri ni mwanzo mzuri, kila mmoja ameona kazi ilivyokuwa, tunaomba
Watanzania waendelee kutusapoti,” alisema Kapombe.
0 COMMENTS:
Post a Comment