September 7, 2015


Pamoja na kupoteza mechi yake ya kirafiki dhidi ya watani wake Coastal Union, African Sports imetuma salamu Msimbazi kwamba wajiandae.

African Sports ambayo imepanda kucheza ligi kuu msimu huu, itakutana na Simba Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mechi ambayo Simba iliyo chini ya kocha wake, Dylan Kerr itataka kushinda ili ionyeshe mwanzo mzuri.

 Katibu wa African Sports, Hatibu Enzi, alisema kuwa hawatishiki hata kidogo kucheza na Simba na kusema kuwa kama wakija kichwakichwa, wanaweza kuondoka na aibu ya mwaka.

Alisema kuwa baada ya kupanda ligi kuu, walifanya maandalizi ya kukutana na timu yoyote ile ya ligi, hivyo hata Simba walishaiweka katika hesabu zao.

“Tulishajua kwamba tutakutana na Simba, hivyo hawatutishi hata kidogo, tunawasubiri tu waje na kama hawajajiangalia vizuri, tutawapiga vibaya mno, wataondoka Tanga na aibu,” alisema Enzi.


Simba, katika mechi zake mbili za mwanzo za ligi, itaanzia kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambako haijawahi kupata ushindi kwenye michuano hiyo. Baada ya kuivaa African Sports, itaikabili Mgambo ambayo msimu uliopita iliifunga Simba mabao 2-0 kwenye uwanja huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic