Mshambuliaji Emmanuel Okwi alilazimika kuvunja mkataba na Simba ili aondoke kwenda Ulaya.
Okwi
amejiunga na timu ya Sonderjyske
inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya klabu hiyo kuelezwa kulipa dola
110,000 (Sh milioni 220).
Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema walimzuia Okwi kuondoka kwa kuwa
hakikuwa kipindi kizuri kumuuza, lakini akaamua kuununua mkataba wake.
“Wale jamaa awali
walitaka kutoa dola 150,000. Lakini tukakataa, unajua ndiyo tunajenga timu na
Okwi alikuwa mchezaji tegemeo. Tukakataa.
“Mwisho Okwi akalazimika
kuununua mkataba wake kama kipengele kimoja ndani ya mkataba kinavyoeleza.
“Kipengele kinaeleza
atoe dola 100,000.
"Akawa ametushinda hata hivyo tukaingia kwenye makubaliano
upya na kufanikiwa kuongezewa anagalau dola 10,000,” alifafanua Hans Poppe.
Hans Poppe alikuwa
akielezea kwamba hawakuwa tayari Okwi aondoke, lakini mkataba ukawabana. Zaidi
soma makala ukuraza wa 12&13.







0 COMMENTS:
Post a Comment