Mshambuliaji
Elius Maguli ambaye kwa sasa anakipiga Stand United ya Shinyanga, amefunguka ya
moyoni kuwa kushindwa kwake maisha ya Simba ilikuwa ni suala la kimbinu kama
ambavyo wachezaji wengi wakubwa wanavyoshindwa katika baadhi ya timu licha ya
kuwa na uwezo mkubwa.
Maguli
amesema kuwa kocha wake wa sasa, Patrick Liewig, anamwamini na anampa nafasi ya
kujiamini zaidi tofauti na ilivyokuwa kwa Kocha wa Simba, Dylan Kerr.
Amesema
kuwa hata Angel Di Maria alishindwa mbinu za Kocha wa Manchester United, Louis
van Gaal, ndiyo maana akahama kwenda PSG lakini haina maana kuwa ni mchezaji
mbaya.
Maguli
ambaye aliachwa Simba licha ya kufunga mabao manne katika mechi za kirafiki,
amesema kuwa kwa sasa amekuwa akijiamini kwa kuwa kocha wake anamwamini pia na
amempa nafasi.
“Yaani
huku sina presha. Bahati nzuri hata kocha mwenyewe ameonekana kunikubali,
katika kila mfumo wake nimekuwa nikisimama katika nafasi yangu kama fowadi wa
mwisho. Anayo mifumo mingi lakini huwa sibadilishwi nafasi, ukweli ni kuwa
tunaelewana vizuri,” alisema.







0 COMMENTS:
Post a Comment