September 1, 2015


Hatimaye mshambuliaji Uhuru Selemani amepata kibali cha kucheza soka nchini Afrika Kusini.


Uhuru amekuwa akisota jukwaani katika kikosi cha Royal Eagles kutokana na suala la kibali cha kufanya kazi nchini humo.


Akizungumza kutoka Darbun, Afrika Kusini, Uhuru amesema sasa mambo ni mazuri.

“Kweli nimepata kibali, ninajisikia faraja sana na uongozi umefanya jambo bora kabisa kwangu.
“Natarajia kushuka uwanjani mechi ijayo. Kwangu ni furaha sana kwa kuwa kila siku nilitamani kuungana na wenzangu kuisaidia timu,” alisema.


Uhuru amejiunga na Royal Eagles kwa mkopo akitokea katika kikosi cha Jomo Cosmo pia cha Afrika Kusini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic