September 1, 2015

MASHALI

Pamoja na kufanikiwa kumshinda bondia Ibrahim Tamba, mkongwe Thomas Mashali amesema, bwan’mdogo huyo ni hatari.


Mashali amekubali kuwamba Tamba ni bondia bora ambaye atasumbua sana hapo baadaye.

Mashali alimshinda Tamba kwa pointi katika pambano lao la raundi 10 lililopigwa juzi kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na ushindi huo, Mashali alikiona cha moto ikiwa ni pamoja na kupasuliwa jicho na Tamba ambaye alikuwa akipambana bila kuchoka.



“Tamba ni bondia mgumu na alijiandaa sana, utaona nilifanya kila linalowezekana lakini aliendelea kupambana.
“Nimeshinda kihalali, kila mmoja ameona. Lakini lazima nikubali bwana mdogo alitoa upinzani mkali,” alisema.


Mashali amesema Tamba anaweza kuwa mmoja wa mabondia bora kabisa kama atajiendeleza vizuri katika mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic