Utani kazi kwelikweli, Msemaji wa
Yanga, Jerry Muro amesema angependa watani wao Simba waanzishe bendi ya muziki
kwa kuwa wanalaumu sana kuhusiana na kufungwa bao 2-0 na Yanga.
Muro amesema anajua Simba sasa
wanaweza kuanzisha bendi ya muziki, anaamini msemaji wa Simba, Haji Manara
ataifanya kazi hiyo vizuri
“Ukiachana na Manara ataweza kuimba,
nimesikia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe yeye ni
mtaalamu wa kupiga gitaa.
“Nampa gitaa katika bendi hiyo ili
afanye kazi yake vizuri, ninaamini ataiweza vizuri,” alisema Muro.
Lakini kwa upande wa Hans Poppe
ambaye amekuwa akiwapa tumbo joto watani wake Yanga, yeye alisema wana hana
hofu kwa kuwa anajua watakutana tena na Yanga.
“Najua tutakutana nao kwa mara
nyingine, nitawapa supu ya aina nyingine, sio ile tena ya mawe na misumari.
“Sasa wana haki ya kusema, lakini
wajue tutakutana nao safari nyingine. Najua tumekuwa tukiwafunga mfululizo kwa
miaka miwili sasa, tuna uwezo wa kuendeleza hilo,” alisema.
Katika mechi hiyo, Simba ilionyesha
soka safi na kuipa Yanga wakati mgumu sana, lakini ikashindwa kutumia nafasi
iliyozipata kupata mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment