Manchester City ni fungu la kukosa kila unapozungumzia
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Leo wakiwa nyumbani Etihad, wamechapwa mabao 2-1 na
mabingwa wa Italia, Juventus.
Juve walianza kujifunga kwa bao la beki Girgio
Chiellini lakini baadaye Juventus wakasawazisha na kuongeza.
Kwanza alianzia Mario Mandzukic kabla ya kijana matata
Alvaro Morata kufanya mambo yake kwa kufunga bao la pili.
Nahodha wa Man City, Vincent Kompany alikuwa nje
akishuhudia jahazi likizama baada ya kutolewa nje kutokana na kuumia.
0 COMMENTS:
Post a Comment