September 21, 2015


Pamoja na Yanga kushinda mechi tatu mfululizo, huku mshambuliaji wake Donald Ngoma akifunga kila mechi, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema Yanga imefanya usajili kama ilivyotaka kwa asilimia 75.


Manji amefanya mahojiano maalum na gazeti hili na kusema, kwa anavyoona, usajili wa Yanga haujawa asilimia 100 kama ambavyo aliamini utakuwa.

Yanga tayari imecheza mechi tatu, ikianza kuitwanga Coastal Union mabao 2-0, ikaikung’uta Prisons 3-0 kabla ya kuiangukia JKT Ruvu kwa mabao 4-1.



Mwenyekiti huyo kijana wa Yanga amesema, anaamini usajili wao umefanikiwa kwa asilimia 75 ingawa kwa wachezaji walionao, wanaweza kuongeza juhudi na kufikia asilimia 100.

“Juhudi za wachezaji walio katika kikosi kwa sasa, inaweza kufanya usajili ufikie yale malengo ya asilimia mia.

“Kwa sasa naweza kusema bado, ni kama mafanikio ya asilimia sabini na tano hivi. Kadiri tunavyokwenda na wachezaji na kocha kama wataongeza juhudi zaidi wakitaka kushinda kila mechi, ninaweza kusema sasa tumefanikiwa kwa asilimia mia,” alisema Manji.

Manji amesema uongozi wa Yanga umekuwa karibu na kamati zote pamoja na benchi la ufundi kwa kuwa unataka Yanga inayofanya vizuri kitaifa na kimataifa.

“Tumekuwa tukifanya vizuri nyumbani, vizuri tukifanya vizuri kimataifa. Ni jukumu la wachezaji kupambana, nasi tuko pamoja nao,” alisema.

Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara na tayari wana mabao nane katika mechi tatu, Ngoma akiwa amefunga matatu.

Tangu Manji amechukua nafasi ya mwenyekiti, Yanga imekuwa ikishika nafasi ya kwanza, yaani bingwa au ya pili na zote imekuwa ikipata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic