September 21, 2015

RUVU SHOOTING KABLA YA KUTEREMKA DARAJA...
Timu ya Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, imeanza vibaya harakati zake za kurudi ligi kuu baada ya kuchapwa bao 1-0 na maafande wenzao wa JKT Mlale ya Ruvuma katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea.


Kichapo hicho kimetia doa mipango ya timu hiyo ambayo ipo kwenye mikakati mizito ya kurudi ligi kuu msimu ujao baada ya msimu uliopita kuporomoka.

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema licha ya kipigo hicho ambacho amekiita cha kushtukiza, kamwe hawatavunjika moyo kwani ni mapema mno.
 “Tumekubali tumefungwa lakini ari yetu ya kucheza ligi kuu msimu ujao ipo palepale, tutajipanga kwa mechi zijazo ili kuhakikisha tunatimiza azma yetu tuliyojiwekea,” alisema Masau.


MATOKEO MENGINE: Friends Rengers 1-1 Polisi Dar, Mbao Fc 2-2 Geita Gold Sports, Polisi Morogoro 1-0 Bukina Faso, Panone 4-0 Oljoro na Lipuli 2-0 Kimondo FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic