Floyd
Mayweather ameendeleza kutoa vipigo kwa kila anayekutana naye baada ya
kumtwanga Andre Berto.
Ushindi wake
dhidi ya Berto umemfanya achukue rekodi ya kucheza mapambano 49 ya ngumi za
kulipwa bila ya kupigwa hata mara moja.
Majaji wote
wamempa ushindi Maywether, wa kwanza akitoa 120-108, wa pili 118-110 na watatu 117-111
na kumfanya aibuke na ushindi wa unanimous decision.
Kutokana na
ushindi huo, Maywether anaendelea kubaki na ubingwa wake wa dunia wa uzito wa
Welter kwa WBC na WBA.


















0 COMMENTS:
Post a Comment