September 13, 2015

Hatimaye, Tottenham imeachana rasmi na mshambuliaji raia wa Togo, Emmanuel Adebayor.


Taarifa kutoka katika klabu hiyo zimeeleza, Adebayor na Spurs wameachana baada ya kufikia makubaliano.

Lakini Adebayor atalazimika kukaa bila ya kuichezea timu yoyote hadi Januari, mwakani litakapofunguliwa dirisha la usajili.

Awali, Adebayor aligoma kuondoka Spurs hadi atakapolipwa pauni milioni 5 kama inavyoeleza katika mkataba wake.

Hata hivyo klabu hiyo iliona fedha hizo ni nyingi sana. Inaelezwa hata katika makubaliano hayo, Adebayor alikubali kutoa punguzo la dola milioni 2.

Ingawa klabu wala Adebayor mwenyewe, hakuna aliyekuwa tayari kweka wazi kuhusiana na hilo.

West Ham United ndiyo inayoonekana kumtaka na kuna uwezekano mkubwa wa kujiunga nayo Januari, mwakani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic