NAFTAL (KATIKATI) AKIFANYA YAKE LIGI KUU KENYA |
Beki wa zamani wa Simba, David Naftal ameendelea
kung’ara katika kikosi cha Kenya Revenue Authority (KRA) na sasa amepania
kuhakikisha wanamaliza Ligi Kuu Kenya wakiwa katika nafasi tano za juu.
Kutoka Kenya, akizungumza na SALEHJEMBE, Naftal
amesema amekuwa akipambana na sasa ana uhakika wa namba katika kikosi cha
kwanza, lakini kwa pamoja KRA wanataka nafasi hizo tano za juu.
“Tupo katika nafasi ya saba ya ligi. Tumebakiza
mechi nne, sasa tunapambana kumaliza katika top 5.
“Huku Kenya mkimaliza top 5, mnapata nafasi ya
kucheza michuano ya Top 8 ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Shirikisho,”
alisema Naftal.
Kwa sasa amekuwa akicheza nafasi ya kiungo
mkabaji nan dye tegemeo katika kikosi hicho cha wakusanya kodi wa Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment