September 15, 2015

MISHETO AKIWA KAZINI NCHINI UJERUMANI...
Kiungo Charles Misheto amefanikiwa kufunga bao la kusawazisha na kuisaidia timu yake ya Rabestein FC kupata sare ya bao 1-1.


Rabestein FC inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Ujerumani, imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya FC Plauen.

FC Plauen iliyokuwa nyumbani ndiyo ilianza kupata bao mapema na kuilazimisha Rabestein FC kupambana kusawazisha.


Juhudiz a Misheto aliyewahi kuichezea Stand United, zilizaa matunda mwishoni kabisa mwa dakika 10 za mwisho alipofanikiwa kusawazisha bao hilo kwa mkwaju safi.


Misheto ni kati ya vijana wa kitandania ambao wamekuwa wakijituma kuhakikisha wanafanikiwa kimaisha. Kabla alitakiwa na klabu ya daraja la tatu, lakini aliamini Rabestein FC inayoshiriki daraja la nne ni njia sahihi kwake kuanza kupanda juu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic