Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/2016
inatazamiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba
kuchezwa katika viwanja tofauti nchini.
Ndanda FC ya Mtwara watakua wenyeji wa Mgambo Shooting
katika uwanja wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana Kimanumanu African Sports
watawakaribisha Simba SC katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wana
Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa
Majimaji mjini Songea.
Azam FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kaika
uwanja wa Chamazi Complex, Stand United FC chama la wana watawakaribisha Mtibwa
Sugar katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Toto Africans watawakaribisha
Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar katika
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumapili Ligi Kuu Bara itaendelea kwa mchezo mmoja tu
utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa
watetezi wa kombe hilo Yanga SC watawakribisha wagosi wa kaya Coastal Union.
Katika hatua nyingine klabu ya Kagera Sugar ya mkoani
Kagera itatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa mechi zake
za nyumbani dhidi ya Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu (Sept 30), Tanzania
Prisons (Oct 4) na Yanga (Oct 31).
Mabadiliko hayo yamefanyika kupisha shughuli
ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea kwenye uwanja wao wa Kaitaba mjini
Bukoba unaofanywa na wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(Fifa).
0 COMMENTS:
Post a Comment