UHURU NA NGASSA WALIPOKUTANA MARA BAADA YA MCHEZO.... |
Mshambuliaji Mrisho Ngassa ameng’ara kwa kuisaidia timu yake
ya Free State Stars kupata ushindi wa mabao 3-2 ikiwa ugenini.
States imeshinda dhidi ya Martizburg, huku Ngassa akitoa
pasi mbili za mabao na kucheza kwa dakika 90.
Wakati Ngassa akifanya yake uwanjani, Mtanzania mwingine
anayecheza Afrika Kusini, Uhuru Selemani alikuwa uwanjani hapo.
Uhuru ameiambia SALEHJEMBE, kwamba Ngassa ameonyesha kiwango
bora kabisa, jambo ambalo ni sifa kwa Watanzania.
“Nimesikia raha sana, Ngassa amecheza vizuri na mimi nikiwa
hapa, nimeona ni sifa kubwa na kitu cha kujivunia,” alisema.
Baada ya mechi hiyo, Uhuru anayekipiga Royal Eagles
alikutana na Ngassa na kubadilishana naye mawazo.
Mabao ya States katika mechi hiyo yalifungwa na Danny Wayne
katika dakika ya 63, Andrea Fileccia dakika ya 81 kwa penalti kabla ya mkali,
Robert Sankara kumaliza kazi katika dakika ya 90.
0 COMMENTS:
Post a Comment