Baada ya kufunga bao lake la kwanza la Ligi Kuu
Bara ikiwa ndiyo mechi yake ya kwanza ya ligi hiyo, Donald Ngoma amesema
ataendelea kuifungia Yanga.
Ngoma raia wa Zimbabwe amesema ana imani kubwa ya
kuendelea kufanya vizuri kutokana na ushirikiano wa kikosi hicho.
“Ninajua mabeki watanipania sana, watataka
kunizuia lakini ndiyo kazi yao. Mimi nitakachofanya ni kufunga kila
nitakapopata nafasi,” alisema.
Ngoma alifunga bao la pili wakati Yanga
ikiididimiza Coastal Union kwa mabao 2-0.
Straika huyo aliyejiunga na Yanga msimu huu
akitokea FC Platnum ya Zimbabwe alionekana kuandamwa na ukame wa mabao wakati
wa mechi za kirafiki zikiwemo zile za Kombe la Kagame ambazo Yanga iliishia
robo fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment