September 8, 2015


Yanga imeamua kubaki Dar es Salaam ili kuepusha kuwachosha wachezaji wake.


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema hakuna sababu ya kusafiri kwenda Bagamoyo pia kuweka kambi huko huku wakifanya mazoezi Dar es Salaam.

“Angalau kuna mambo  tunaweza kuyaepuka ambayo yangeongeza tu uchovu kwa wachezaji.

“Mechi yetu na Coastal Union itakuwa Dar es Salaam, naona itakuwa vizuri tukamalizia maandalizi yetu hapa na kuanza ligi mara moja bila ya mizunguko,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi.


Yanga itaanza kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara kwa kuwavaa Wagosi wa kaya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa ambajo itachezwa Jumapili ijayo, siku moja baada ya msimu wa 2015-16 kuanza rasmi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic