September 5, 2015

PONDAMALI (KULIA) AKIWA NA SALEH ALLY (KATIKATI) NA PHILLIP EPAFRA NKINI WA CHAMPIONI. WANIGERIA WANAMTAFUTA PONDAMALI...

Dakika chache tu mara baada ya kushuka kwende ndege, mabosi na mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria, jina la kwanza kulitaja ni Juma Pondamali ambaye ni kocha wa makipa wa Yanga.


Wakiwa katika msafara wa watu 150, mashabiki hao waliotua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere usiku wa kuamkia jana saa 6:10 kwa ndege binafsi kutoka nchini mwao walikuwa wakimuulizia Pondamali kwa watu wa uwanjani hapo.

Nigeria imekuja kucheza mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika 2017 dhidi ya Taifa Stars, leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushangiliaji wa Super Eagles aliyejitambulisha kwa jina la Dk. Orabiko alisema: “Pondamali yupo wapi? Tungependa kukutana naye.

“Tunamjua kuwa alikuwa kipa wa zamani wa timu ya taifa (ya Tanzania), Pondamali hivi bado yupo? Yule tunamkumbuka kwa mengi sana hasa vituko vyake.


“Ni kipa mwenye vituko vingi akiwa golini ambaye pia alitusumbua sana kwenye mechi yetu tuliyocheza Lagos, ana jina kubwa nchini kwetu, tunaomba atutembelee hotelini kwetu tupige naye picha za kumbukumbu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic