Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mukangara
kesho Jumapili, Septemba 13, 2015 saa 8 kamili mchana anatarajiwa kuzindua
rasmi fainali za michuano ya Airtel Rising Star katika uwanja wa Karume jijini
Dar es salaam.
Jumla ya timu sita zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ambayo imekua
ikifanyika kila mwaka nchini kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel, ambapo vijana wenye vipaji huchaguliwa na kupata nafasi ya kujiunga na
vituo vya michezo (Academy) za Dakara – Senegal na Doha – Qutar zinazomilikiwa
na kampuni hiyo.
Katika uzinduzi huo wa kesho, timu za mkoa wa Ilala, Kinondoni, Mbeya,
Morogoro, Mwanza na Temeke zinatarajiwa kupambana kusaka mshindi kwa fainali
hizo za kitaifa.







0 COMMENTS:
Post a Comment