September 13, 2015

PLUIJM...

Yanga kulitetea Kombe inalolishikilia la Ligi Kuu bara kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union.


Kwa ushindi huo wa mabao mawili na kupata pointi tatu, Yanga inayonolewa na Mholanzi, Hans van der Pluijm inakaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara.

Yanga imepata ushindi huo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku mabao yote yakifungwa katika kipindi cha kwanza.

Simon Happygod Msuva na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe ndiyo waliofunga mabao hayo mawili ya Yanga.

Ahmed Shiboli wa Coastal Union alipoteza nafasi tatu safi za kufunga ambazo zingewasaidia angalau kupata bao la kufutia machozi au kusawazisha zaidi.

Yanga bao walipoteza nafasi nyingine tatu kupitia Amissi Tambwe, Msuva na Haruna Niyonzima.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanaungana na Simba, Toto African, Majimaji, Azam FC, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kuwa timu zilizoanza na ushindi katika siku ya kwanza ya ligi.

Leo kulikuwa na mechi hiyo moja kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union wakati pazia la ligi hiyo lilifunguliwa jana kwa mechi saba kuchezwa.

MECHI ZA JANA:
African Sports 0-1 Simba
Majimaji 1-0 JKT Ruvu
Azam FC 2-1 Prisons
Stand Utd 0-1 Mtibwa
Toto 1-0 Mwadui

Mbeya City 0-1 Kagera

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic