Uhuru Selemani ameanza kazi nchini Afrika Kusini
wakati timu yake ya Royal Eagle ikiichapa Amazelu kwa mabao 2-1.
Raha zaidi, ikiwa ndiyo mechi yake ya kwanza,
Uhuru amefanikiwa kufunga bao la ushindi.
“Nina furaha sana, ni mechi ya kwanza ya ligi,
nimefanikiwa kufunga bao la ushindi,” alisema Uhuru alipozungumza na
SALEHJEMBE.
Kabla ya hapo, Uhuru hakucheza mechi takribani
tatu kutokana na kutokuwa amepata kibali cha kufanya kazi.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, amesajiliwa
na Jomo Cosmos kabla ya kupelekwa kwa mkopo Royal Eagles yenye makao yake makuu
jijini Durban.








0 COMMENTS:
Post a Comment