October 27, 2015


NA Mwandishi Wetu
Straika wa Simba, Hamis Kiiza, anatarajiwa kukabidhiwa zawadi yake ya Sh milioni 1 ya Mchezaji Bora wa Mwezi na wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, baada ya kuibuka kidedea Septemba.

Kiiza alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Septemba baada ya kufanya vema katika mwezi wa kwanza wa ligi hiyo, akiisaidia timu yake ya Simba kushinda mechi tatu mfululizo, huku Mganda huyo akifunga mabao matano, ikiwamo ‘hat-trick’ katika pambano dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, Kiiza atakabidhiwa kitita chake hicho na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao, wakati wa mchezo wa Simba dhidi ya Majimaji Oktoba 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Alisema kuwa kampuni yao itaendelea kutoa zawadi kwa wachezaji wanaofanya vizuri kila mwezi, ikiwa ni sehemu ya mikakati na mchango wao katika kuinua kiwango cha michezo, hususan soka nchini na kubadilisha maisha ya wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu.
“Katika kuendeleza mikakati yetu ya kuinua soka hapa nchini pamoja na kuboresha maisha kwa wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Vodacom Tanzania, itamjaza kiasi cha Sh milioni moja mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza kutokana na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa ligi hiyo kwa Septemba msimu huu,” alisema Nkurlu.
Juu ya tuzo hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ameishukuru na kuipongeza Vodacom Tanzania ubunifu huo wa kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri kwani kitendo hicho huchangia kuendeleza vipaji na kuwahamasisha wachezaji kufanya vizuri zaidi na kuzisaidia timu zao.

“TFF tunaamini zawadi kama hizi zinazotolewa kwa Mchezaji Bora wa Mwezi, zinaweza kuwa chachu kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu kujituma zaidi kwa faida yao, klabu zao na soka la Tanzania kwa ujumla,” alisema.
Tangu tuzo hiyo ianze kutolewa Septemba mwaka jana, ni Coastal Union pekee iliyofanikiwa kutoa wachezaji wawili walioibuka kidedea hadi sasa.

Washindi wa tuzo hiyo tangu ianzishwe mwaka jana ni Antony Matogolo wa Mbeya City (Septemba, 2014), Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr’ (Azam FC, Oktoba), Rashid Mandawa (Kagera Sugar, Novemba), Joseph Mahundi, Said Bahanunzi (Polisi Moro, Januari) na Godfrey Wambura (Coastal Union, Februari), 
James Mwasote (Police, Machi) na Mrisho Ngassa (Yanga, Aprili).


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic